Watu wengi hupata chunusi, vipele, ngozi kukauka na matatizo mengine katika ngozi zao kwa sababu ya kutumia losheni au mafuta ambayo hayaendani na ngozi zao. Hii huweza kusababishwa na ushauri mbaya kutoka kwa wauzaji wasiojua vizuri vipodozi au kwa wanunuaji wenyewe kutojua vizuri vipodozi.

Ukitaka matokeo mazuri kwenye ngozi na mwili wako kwa ujumla hakikisha unazingatia mambo yafuatayo:
  1. Unaitunza ngozi yako vizuri sana kupitia usafishaji mzuri, ulaji mzuri, kuipumzisha, kuepuka jua kali, kunywa maji ya kutosha, unatumia vizuri vipodozi nk
  2. Unatumia vipodozi vinavyoendana na ngozi yako na mahitaji yako
  3. Unatumia vipodozi vilivyo salama na vyenye ubora wa hali ya juu
Kwa upande wa kuchagua vipodozi vinavyoendana na ngozi yako naomba leo tukufafanulie vizuri ili usipate matatizo tena au kudanganywa na muuzaji wa vipodozi asiye na elimu na ujuzi wa kutosha
AINA ZA NGOZI

Kwanza jua vizuri sana aina ya ngozi yako. Jijue kama una Ngozi kavu (Dry Skin), Ngozi ya mafuta (Oily Skin), Ngozi ya Kawaida (Normal Skin) au Ngozi mchanganyiko (Combination Skin).
Unaweza kujua aina ya ngozi yako kwa kuichunguza wakati wa asubuhi baada ya kuamka au baada ya kuoga na kukaa muda kidogo bila kupaka mafuta.
Ngozi kavu hukakamaa, hupauka, huwa na magamba kwa mbali na haitoi mafuta yoyote. Ukijifuta kwa karatasi nyeupe au ukitumia karatasi ya kupimia ngozi hutoka kavu kabisa na haina matone ya mafuta
Ngozi ya mafuta huwa tepetepe na hujaa mafuta hata kama haujapaka chochote, Ukijifuta kwa karatasi nyeupe au ukitumia karatasi ya kupimia ngozi hutoka na matone mengi ya mafuta ambayo yameungana au yapo karibu karibu
Ngozi ya kawaida huwa kati ya kavu na ya mafuta. Yaani haioneshi mafuta mengi na wala sio kavu. Ukijifuta kwa karatasi nyeupe au ukitumia karatasi ya kupimia ngozi hutoka na matone machache ya mafuta ambayo yapo mbalimbali
Ngozi mchanganyiko ni ile ambayo sehemu huwa kavu na sehemu huwa ya mafuta. Yaani eneo la kutokea kwenye paji la uso na kushuka kupitia kwenye pua (T-Zone) huwa ya mafuta na mashavu huwa ngozi kavu. Ukitumia karatasi nyeupe au karatasi ya kupimia ngozi hutoka na mafuta eneo kutokea kwenye paji la uso na kushuka kupitia kwenye pua (T-Zone) na hutoka kavu eneo la mashavu.
LOSHENI/MAFUTA YA KUTUMIA
Hapa ndipo penyewe. Na ukikosea hautapata matokeo unayoyataka, sana sana utapata matatizo na kupoteza muda na pesa zako.
Kwanza kabisa tambua kwamba losheni na mafuta mengi sana hufanya kazi zinazofanana na hata ufanisi wao hufanana, tofauti zao kubwa ni harufu tu na bei. Kwa hiyo cha muhimu kuzingatia ni aina ya ngozi yako na malengo ya hiyo losheni au mafuta yako.
Tuna mafuta na losheni aina nyingi sana. Zote huwa na mapambo na matangazo aina mbalimbali, ukiongezea na promosheni na maneno ya wauzaji.
Miluzi mingi hupoteza mbwa, ila wewe sio mbwa na usipotee sasa.
  1. Ngozi ya Kawaida
Ngozi ya kawaida ndiyo ngozi nzuri kuliko zote. Siku zote lenga kuwa na ngozi hii ili maisha yako yawe mazuri na kutunza ngozi yako kuwe rahisi.
Kama una ngozi ya kawaida tumia mafuta au losheni mahsusi kabisa kwa ajili ya ngozi ya kawaida. Huwa zimeandikwa “NORMAL SKIN” au “FOR NORMAL SKIN”.
2.  Ngozi ya Mafuta 
Ngozi ya mafuta ipo katika hatari ya kupatwa na chunusi na kusumbuliwa na vumbi na vijidudu. Haihitaji sana mafuta, ila cha msingi ni kuhakikisha haipotezi maji na hakuna chunusi. Kama una ngozi ya mafuta anza kupunguza mafuta na kuifanya iwe ya kawaida ili maisha yako yawe mazuri na kutunza ngozi yako kuwe rahisi.
Kwa upande wa mafuta/losheni tumia yaliyo mahsusi kabisa kwa ajili ya ngozi ya mafuta. Huwa yameandikwa “OILY SKIN” au “FOR OILY SKIN”.
Ukianza kutafuta mafuta/losheni hizo utakuja kugundua kwamba ni adimu sana. Hii ni kutokana na ukweli kwamba ngozi ya mafuta haihitaji sana mafuta au losheni, na badala yake huhitaji vipodozi vingine kabisa kwa ajili ya kupunguza mafuta na kuifanya iwe ya kawaida.
3.  Ngozi Kavu
Ngozi kavu ipo katika hatari ya kupata magonjwa ya ngozi, kuchanika na kuwahi kuzeeka. Inahitaji sana unyevuunyevu na mafuta kuliko ngozi yoyote. Ngozi kavu ni tatizo, hakikisha unaondokana nayo haraka iwezekanavyo.
Tumia mafuta au losheni ambazo ni mahususi kabisa kwa ajili ya ngozi kavu. Na kama ngozi yako ni kavu sana tumia mafuta au losheni kwa ajili ya ngozi kavu sana.
Tumia mafuta/losheni zilizoandikwa “FOR DRY SKIN” au “DRY SKIN”. Kama ngozi ni kavu sana tumia mafuta/losheni iliyoandikwa “FOR VERY DRY SKIN”.
4.  Ngozi Mchanganyiko
Ngozi hii ni hadimu na haina matatizo sana. Cha msingi ni kupata mafuta/losheni mahususi kwa ajili ya ngozi hii na kuitunza vizuri ili iweze kunawiri.
Endapo mafuta eneo la pua yatakuwa mengi au yanakusumbua sana basi unaweza ukayapunguza kwa kutumia vipodozi vya kupunguza mafuta na kuwa na amani zaidi.
Kwa upande wa mafuta/losheni tumia yaliyoandikwa “FOR COMBINATION SKIN”
Baada ya hapo maisha yako yatakuwa poa kabisa.
MAFUTA/LOSHENI KWA AJILI YA ZAIDI YA AINA MOJA YA NGOZI
Kuna mafuta na losheni ambazo zimetengenezwa kwa ajili ya aina mbalimbali za ngozi. Endapo utaweza kujaribu kwa muda kutazama maendeleo na kuwa na uhakika nayo basi yanaweza kukufaa pia.
Baadhi yao huwa ni kwa ajili ya Ngozi kavu mpaka za kawaida. Haya utakuta yameandikwa “FOR DRY TO NORMAL SKIN” au “FOR DRY AND NORMAL SKIN”
Baadhi yao huwa ni kwa ajili ya ngozi kavu mpaka kavu sana. Haya utakuta yameandikwa “FOR DRY TO VERY DRY SKIN” au “FOR DRY AND VERY DRY SKIN”
Baadhi yao huwa ni kwa ajili ya ngozi mchanganyiko mpaka za kawaida. Haya utakuta yameandikwa “FOR COMBINATION TO NORMAL SKIN” au “FOR COMBINATION AND NORMAL SKIN”ngozi 1
Nina imani sasa utakuwa umeelewa vizuri sana na utaweza kuchagua vizuri mafuta/losheni na kushauri watu.  Na next Monday ntaendaa ongelea namna ya kutunza aina hizo za ngozi ya uso thaaanksss and GOD BLESS YOU
Wakati watu wengi wakitumia mafuta pia na lotion zenye viambatana sumu yani kemikali na kuharibu ngozi zao za uso (reception) but Kuna njia za asili na za kuaminika za kuondoa chunusi na hazihitaji pesa nyingi kutumia

1.Kipande cha barafu 
Barafu husaidia kukausha/kunyausha chunusi  na kunyonya mafuta na kuyasambaza katika maeneo mengi ya mwili

Namna ya kutumia
Chukua barafu tia kwenye kitamba safi then fanya kama una massage sehemu yenye chunusi
Fanya mara nyingi uwezavyo

2.Asali
Pia imethibitishwa na wataalam wa ngozi kuwa asali inasaidiaa sana kuondoa chunusi kwa kuzibua matundu ya hewa ya ngozi na kufanya ngozi kupumua vizuri , endapo matundu yakizipa husababisha chunusi

Namna ya kutumia
Tumia pamba safi chovya asali paka katika eneo lenye chunusi fanya kama unamassage eneo, acha kwa dakika 10  osha kwa maji ya uvuguvugu

3.Maji ya limao (lemon juice)
Linauwa vijidudu katika ngozi pia huondoa chunusi haraka kwa sababu ya kemikali zipatikanazo ndani yake

Namna ya kutumia
 Tumia pamba safi weka kwenye eneo lenye chunusi  baadaa ya hapo lala mpaka asabuhi , nawa uso uamkapo

4.Dawa ya Meno
Dawa ya maajabu ya kuondoa chunusi haraka bila kuacha kovu, inakausha chunusi haraka sana

Namna ya kutumia
Chukua dawa kidogo weka eneo lenye chunusi mpaka asubuhi then nawa uso kwa maji safi

5.kitungu Swahumu
Kitungu hutibu magonjwa takribani 20 pia chunusi kwa uharaka sana

Namna ya kutumia
Kata kitungu swahumu vipande viwili
Sugua taratibu eneo lenye chunusi

6.chapa maandashi(baking powder)
Pia namna nyingine ya kuondoa chunusi, inasaidiaa kunyonya mafuta uso haraka sana na kuacha uso ukiwa mkavu na nyororo

Namna ya kutumia
-kijiko cha chai kimoja Cha chapa mandashi
-Maji kiasi au maji ya limao
-changanya
-Osha uso
-Paka mchanganyiko wako subili kwa dakika 5
-Osha uso kwa maji ya uvuguvugu
Kwa maswali,ushauri please put your comments asanteee sana





Avocado ni tunda ambalo limesheheni potassium,amino acids,na pia protein ambavyo ni muhimu katika mwili wa binadam
But Leo ntazungumzia sana umuhimu wa avocado katika nywele pia namna ya kuapply katika nywelee

Najua Dada zetu mwengi wanapenda kuwa na African natural hair ambazo zinamuonekano mzuri na za kung'ara, avocado ni jibu lako.

FAIDA ZA PARACHICHI KATIKA NYWELE

Moisturisers hair(unyevu katika nywele)



Husaidia nywele kuwa nyevu wakati wote pia zenye mwonekano mzuri, pia hazina ugumu wakati wa kuchana

Faster growth of hair (hukuza nywele haraka)


Kulingana na zitu zilivyo kwenye parachichi husaidia kukuza nywele haraka sana

Protect against dandruff(kuzuia/kuondoa mmba


Mmba kichwani inamaana ngozi yako ya kichwa haina mafuta yani ikavu so parachichi husaidia kuongeza mafuta kwenye ngozi yako ya kichwa

Rejuvenates hair(hufufua nywele)


Pia linasaidia kufufua nywele kwa Wale waliokatika nywele wenye vipara

Namna ya kutengeneza mchanganyiko WA parachichi

Parachichi moja +Nazi changanya then apply kwa nywele wait for at least 10 minutes and above then osha nywele zako. Kumbuka usichane nywele zikiwa mbichi kwa sababu nywele zikiwa mbichi huwa dhaifu
 Thaaaaankssssss for viewing and please put some comment





An amazing praising gospel music just click link below to download and to watch it and I promise you utaenjoyy wimbooo amazing from my best friend imma vistor fromm mwanza

. https://drive.google.com/file/d/0BxNEfOZMxaXEN0RXSVROdjkxOU0/view?usp=drivesdk
Leo nimeona niaaanzeee na ndugu zanguu waislamm coz wako katika mfungu wa Ramadan sooo hopee utaenjoyy coz nakupa full package.

Ramadan inajulikana kuwa ni mwezi mtakatifu kwa ndugu zetu waislamm when they take religion seriously but no one said huwezi kuwa fashionable and styled in Ramadan 
Sooo zifuataazooo ni five accessories(vivalio) ambavyoo you must have in ramadan

HAT



Hijab & hats, yecc perfect comboo na kama wajua namna yakumatch , pia chaguaa hat ambayoo inaweza kueendana na your outfit
Hebu try na uupe muonekano wako a classy touch

SUNGLASSES


Are valuablee fashion accessories for women and men but siyo tu fashion accessories but inadecens taste, lakini kwenye sunglasses chagua kulingana na shape ya uso wako 

NECKLACES

Necklacess(cheni) mmh unawezaa  add some necklaces on your outfit ,but kwa black hijab inapendezeaa Sanaa golden necklaces I promise you you will look amazing

EARRINGS

Yaaah earring pimp your look by adding some earingg Tena zitakazoo endaaanaa Sanaa na your outfit kama our sister hapo beyoncee,  also try ziwepana kidogoo ilizionekane vizuri

BELTS/WAIST BELT

Belts yaaah kuadd something on your look ambayoo itakuonesha fashionable like black hijab and golden belt pia inasaidiaa kuonesha shape kidogoo

PASHMINA

Pashmina in Swahili ni mtandiooo unamatumizi mengi sana unawezaa fungiaa kilembaa or ukatumia kama skafuu and ECT(head wrap,shawl, even hijab style)

Thaaanksss sana kwa kuview my blog kwa any comment pleasee put some comment mawazoo wako means a lot to me


My dear viewer's on every Monday I will be posting style and life's tips .........soooo (jiaaandaaaeeee itakuwaaaaa hoooot Sanaa much love 2 u)😘